33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kisa Chama,Simba yaijia juu Yanga

ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Simba umeibuka na msimamo kuwa kiungo wao Mzambia Clatous Chama kamwe hawezi kujiunga na watani zao wa jadi Yanga hata kama wataamua kuvunja ‘ benki’ kwa kumtangazia dau kubwa.

Msimamo wa Wekundu hao umekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za chini  chini kuwa, Yanga inavutiwa na Chama na imedhamiria kumng’oa Mzimbazi.

Habari za Yanga kumwitaji Chama zilikolewa na nyingine iliyoeleza kuwa kiungo huyo hana furaha ya kuendelea kucheza Msimbazi, licha ya kwamba ni miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, aliandia: ” Litakuwa jambo la kushangaza Chama kwenda ‘Utopolo FC’(anamaanisha Yanga), waache vibweka wapuyange na hadithi za kuku mjamzito.

“Yaani mchezaji mwenye akili anayejua maisha ahame Simba kwenda kucheza Utopolo lands,thamani ya Chama sio ya kucheza timu isiyocheza Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Wakati Manara akiandika hivyo,Mtendaji Mkuu wa Simba,Senzo Mbatha,aliliambia MTANZANIA  jana kuwa, ni vigumu kwa Yanga kumsajili Chama bila ya kukaa meza moja na Simba.

“Baada ya ligi ya msimu ulioisha kumalizika, kuna wachezaji tuliwaongezea mkataba, akiwemo Chama ambao utaisha msimu wa 2020/21, hivyo Yanga watawezaje kumsajili, labda wavunje mkataba na hilo hadi Simba tukubaliane nao.

“Bila shaka wanacheza tu na akili za wanachama wao kuwaaminisha jambo ambalo haliwezekani kutokea.

“Wache kuwaaminisha wanachama wao kitu cha uongo, kufanya hivyo kutawajengea taswira mbaya na kutoaminika hata katika jambo lenye

ukweli, binafsi najua wachezaji ambao Yanga itawasajili haiwezi kuwatangaza hadi pale watakapokamilisha mipango yote, yeyote atakayetajwa kabla hajasajiliwa, hawataweza kumsajili,” alisema Senzo.

“Wache kuwaaminisha wanachama wao kitu cha uongo, kufanya hivyo ni kutawajengea taswira mbaya na kutoaminika hata katika jambo lenye ukweli, binafsi najua wachezaji ambao Yanga itawasajili haiwezi kuwatangaza hadi pale watakapokamilisha mipango yote, yoyote atakayetajwa kabla hajasajiliwa hawatoweza kufanya hivyo,” alisema Senzo.

Tayari imeelezwa kuwa uongozi wa Simba umeanza mchakato wa usajili kimya kimya, huku ukijiandaa kumalizana na wale ambao hawapo katika mpango wa kocha wao, Sven Vandenbroeck.

Imeelezwa kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ndani ya klabu hiyo ni hatima ya Ligi Kuu Tanzania Bara kama itaendelea au itavunjwa kutegemea mwenendo wa janga la virus vya ugonjwa wa Corona unaoitesa Dunia kwa

sasa.

Ligi za mataifa mbalimbali zimesimamishwa kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya Corona vinavyoendelea kusababisha vifo, huku kukiwa na kesi kibao za waathirika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles