WELLINGTON, New Zeiland
WAZIRI anayeshughulikia masuala ya wanawake nchini hapa amelazimika kuendesha baiskeli kwenda hospitali kwa wiki 42 kwa ajili ya kujiandaa kujifungua mtoto wake wa kwanza kwa kile ambacho anadai hawakuwa na nafasi ya kutosha ndani ya gari lao na mumewe kwa ajili ya watoa huduma.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Waziri huyo kutoka chama cha Green, Julie Genter, alisema mbali na kukosekana nafasi katika gari hilo, alilazimika kutumia usafiri huo ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kijiweka vizuri katika nafya.
Kupitia ujumbe na picha ambazo azilizutuma jana katika mtandao wake wa jamii wa Instagram aliandika kwamba yeye na mumewe walikuwa wanaifurahia asubuhi hiyo njema.
“Kitu hiki ndicho kinachotupa bahati,” aliwaandikia wafuasi wake kupitia mtandao huo wa jamii.
“Mimi na mume wangu tulipanda baiskeli kwa sababu hapakuwa na nafasi ya kutosha katika gari kwa ajili ya wafanyakazi wa msaada … lakini pia iliniweka mimi katika hali nzuri zaidi.
“Safari ya kutumia baiskeli ya umeme ilikuwa ni nzuri kwa kiasi kikubwa naifurahi safari hii na tunatarajia kuongeza nafasi nyingine kwenye baiskeli yangu kwa ajili ya mtoto atakayekuja wiki chache zijazo,”aliongeza.
Endapo atajifungua waziri huyo ambaye atachukua miezi mitatu kwa ajili ya mapumziko atakuwa ameongeza idadi ya wanasiasa ambao wamejifungua wakiwa madarakani.
Mbunge wa kwanza nchini hapa kujifungua ilikuwa ni mwaka 1970 na mwingine mwaka 1983.
Mwaka 2016 Australia ilibadilisha sheria zake kwa kuwaruhusu viongozi wanawake kunyonyesha wakiwa ndani ya bunge.