25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watuhumiwa wa uhamiaji haramu 314 wakamatwa Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge amesema Katika operesheni ya pamoja iliyofanywa na Vyombo vya ulinzi na usalama Kata ya Mabwepande Januari 24 na 25 imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 314 wa uhamihaji haramu ambapo baada ya kuhojiwa watuhumiwa 84 walibainika kuwa ni wahamiaji haramu.

RC Kunenge amesema Katika watuhumiwa hao 79 wanatokea Burundi, Malawi 02, DRC Kongo 02 na mmoja kutoka Msumbiji ambapo amebainisha watuhumiwa hao wote watafikishwa mahakamani kwa kosa la kuishi nchini kinyume na sheria.

Aidha, RC Kunenge amesema watuhumiwa wengine 33 bado wanaendelea kuchunguzwa uraia wao huku wengine 197 waliobaki waliachiliwa baada ya kubainika kutokuwa na dosari Katika uraia wao.

Hata hivyo RC Kunenge amebainisha kuwa Katika uchunguzi ukiofanyika baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa na viashiria vya kujihusisha na uhalifu wa Wizi, Unyang’anyi, Uporaji wa ardhi na kuuza kwa utapeli pamoja na kuzuia wamiliki halali wa ardhi kuingia Katika maeneo yao Jambo linalozua migogoro ya ardhi.

Sanjari na hayo RC Kunenge ametoa wito kwa wakazi wa eneo husika kuendelea kushirikiana na Vyombo vya ulinzi na usalama Katika kuwafichua wahalifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles