26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Staki upatanishi na upinzani- Museveni

Kampala, Uganda

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameonya watu wenye lengo la ‘kumpatanisha’ yeye na upande wa upinzani baada ya kumalizika uchaguzi mkuu uliompa ushindi kuongoza muhula wa sita.

Huku upande wa upinzani unaoongozwa na msanii, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine aliyeshika nafasi ya pili miongoni mwa wagombea 11 akipinga vikali kutambua matokeo hayo.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuibuka wasiwasi kwa taifa na baadhi ya viongozi wa dini kuomba maridhiano kwa serikali na upinzani.

Katika maadhimisho ya miaka 35 ya chama cha NRM kuingia madarakani yaliyofanyika Ikulu ya nchi hiyo siku ya Jumanne, viongozi wa Kanisa Katoliki katika sala ya kuliombea taifa, waliomba Rais Museveni kufanya maridhiano na kumuachia kiongozi wa chama cha upinzani cha NUP, Robert Kyagulanyi aliyekuwa amezuiliwa nyumbani kwake.

Rais Museveni aliwajibu akisema, serikali ya NRM tayari ilianza maridhiano miaka mingi iliyopita ndio sababu katika serikali yake kuna mwana wa aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin, mwanae Rais wa zamani Tito Lutwa Okello na wengine wengi.

”Fikiria kuna baadhi ya watu wanaokuja kwangu wanataka kuwa wapatanishi wangu na upande wa upinzani, ‘kunipatanisha’ nini? sitaki ‘upatanishi’ wowote.

”Kila mtu anafahamu mahala pangu na mimi ninafahamu mahali upinzani wanapopatikana ninaweza kwenda kwao tukazungumza, sitaki upatanisho wowote, ni matusi kuniambia unataka kunipatanisha,” amesema Museveni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles