24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

WATU WEUSI WALIOFANYA MAAJABU KATIKA MASUALA YA UBUNIFU ULIMWENGUNI

Na JOSEPH LINO


 

WIKI hii tunaendelea kuelezea watu weusi walivyochangia katika uvumbuzi wa teknolojia ambayo leo hii imekuwa chanzo cha maendeleo duniani.

 

Watu weusi waliokwenda utumwani hawakupoteza fursa katika shughuli walizokuwa wanafanyishwa kwa mateso viwandani hadi nyumbani kwa mabosi wao.

 

Walifanya uvumbuzi wa ajabu katika dunia lakini kutokana na ubaguzi miaka hiyo, iliwawia vigumu kutambulika au kupewa haki miliki ya uvumbuzi wa vitu vilivyokuwa vinagunduliwa.

Marekani kwa muda mrefu imekuwa ya kuvumbua vitu tangu miaka 13,000 iliyopita. Moyo wa ubunifu wa Wamarekani umekuwa ukiendelea kizazi hadi kizazi, ambapo hatimiliki ya kwanza ilitolewa mwaka 1641, hadi leo hii wanaendelea kutambua na kutoa hati miliki ya uvumbuzi, maboresho na ubunifu wowote.

Ingawa kundi la watu weusi ambao wamebuni na kuvumbua vitu muhimu kuliko Wazungu wenyewe, katika historia ya Marekani walikuwa wanakataliwa hasa Wamarekani weusi waliozaliwa utumwani.

Lakini sheria ya hatimiliki ya mbunifu wa kwanza (patent law) wa kitu fulani ilianzishwa ambayo ilikuwa haiangalii ubaguzi wa aina yoyote, ndio maana leo watu weusi waliovumbua vitu na kupewa hati miliki ya uanzilishi hadi leo hii ukoo na familia wanafaidika kwa namna moja au nyingine.

Sheria ya hatimiliki Marekani miaka hiyo ya utumwa ilikuwa haitambui watumwa kutoka Afrika ambao wamezaliwa huko kuomba hatimiliki au kumiliki kitu chochote, ambapo mwaka 1857 tume ya Marekani ilipitisha sheria ya mtumwa kutopewa hatimiliki yoyote.

Lakini karne ya 17 na 18 ilikuwa ya mapinduzi ya ukuaji wa uchumi wa Marekani hasa katika viwanda, ambapo watu weusi waliokuwa watumwa walichangia kuvumbua vitu vingi kwenye uchumi wa Marekani ingawa hawakupewa hatimiliki yoyote.

Isipokuwa mtu mweusi akibuni kitu hatimiliki ilikuwa inaenda kwa bosi wa mtumwa au anayemiliki.

Wazungu wengi ambao walikuwa wanamiliki watumwa wengi walinufaika kupitia watumwa wao ambao walibuni vitu vya maendeleo na bado wanaendelea kufaidika hadi leo hii.

Baada ya miaka kadhaa, mchakato wa hatimiliki ulianza kutumika kwa watu weusi, kuanzia kwa Thomas Jennings ambaye alikuwa mtu kwanza kuipata mwaka 1821 baada ya kubuni mashine ya kufulia (dry cleaning) na akafuatia  Norbert Rillieux ambaye alifanya mapinduzi katika kiwanda cha kuzalisha sukari baada ya kubuni mashine ya kuchuja miwa mwaka 1840.

Nafasi hiyo kwa watu weusi imeendelea na hivyo kutambulika hadi leo hii ambapo watu kama Lonnie Johnson ambaye alitengeneza mauzo ya zaidi ya Dola za Marekani bilioni moja sawa na Sh trilioni 2.2, baada ya kubuni kifaa cha kuchezea watoto cha water toy gun (Super Soaker) tangu 1991, kwa mfufulizo kimekuwa miongoni mwa mauzo bora ya ‘toy’ na hadi leo Johnson amepewa hatimiliki zaidi ya 80 ya Green Technologies.

Leo hii kijana wa Marekani anayejulikana kama Bishop Curry V mwenye umri wa miaka 10, amebuni kifaa cha kuzuia vifo kwa watoto vinavyosababishwa na joto kwenye gari baada ya kufungiwa kwenye gari na wazazi wao.

Kijana huyu ametuma maombi ya hatimiliki ya kifaa hicho. Wiki ijayo tutaendelea kuelezea baadhi ya watu weusi waliofanya maajabu katika masuala ya ubunifu ulimwenguni kabla dunia kutambua mchango wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles