29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 25 wauawa, kujeruhiwa kwenye alipuko

MOGADISHU, SOMALIA

DURU za habari nchini Somalia zimeripoti kujiri mlipuko wa bomu Jumapili usiku katika mji wa Baidoa, Kusini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti, bomu hilo lililipuka wakati wa sherehe za Idul-Fitr katika mji huo. 

Aidha duru za habari ziliarifu kwamba katika hujuma hiyo kwa akali watu watano wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa. 

Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo, ingawa inadhaniwa kwamba kundi la kigaidi la al-Shabab ndilo lililotekeleza jinai hiyo.

 Kundi la al-Shabab lenye mfungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaedah hadi sasa limehusika na utegaji mabomu na mashambulizi mengi ndani ya Somalia na katika nchi jirani.

Aidha kundi hilo limekuwa likifanya juhudi za kuiondoa madarakani serikali ya Somalia kuanzia mwaka 2007. 

Hata hivyo mwaka 2011 kundi hilo lilitimuliwa kutoka mjini Mogadishu na jeshi la serikali kwa kushirikiana na askari wa Umoja wa Afrika (AMISOM). 

Pamoja na hayo, bado limeendelea kudhibiti maeneo mengi ya vijijini nchini Somalia. 

Nchi hiyo ni moja ya nchi masikini zaidi na isiyo na uthabiti duniani.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles