Na ABDALLAH AMIRI
-IGUNGA
ZAIDI ya watoto 395,292 katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wenye umri kati ya miaka mitano hadi 14, wamepewa chanjo za magonjwa ya trakoma, kichocho, mabusha na matende pamoja minyoo ya tumbo kwa lengo la kukabiliana na magonjwa hayo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Boranja Semvura, alisema watoto hao ambao wapo shule ya msingi, 137 kati yao wasichana ni 204,151 na wavulana ni 191,141 sawa na asilimia 86 wote walipata chanjo ambayo itasaidia kuimarisha afya zao.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jitegemee, Michael Ernest, alisema kutokana na kujipanga walikamilisha utoaji wa chanjo hizo kwa kufuata taratibu na kanuni zilizotolewa na wataalamu wa afya.