28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

NEYMAR AMKATAZA COUTINHO KUSAINI BARCELONA 

SAO PAULO, BRAZIL

KLABU ya Barcelona inapambana kuhakikisha inaipata saini ya kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutihno, kabla ya kufungwa kwa usajili kesho, lakini taarifa kutoka gazeti la Estadao la nchini Brazil, zinasema Neymar anamshawishi mchezaji huyo asijiunge na Barcelona.

Tangu msimu huu wa ligi kuu uanze, Coutinho bado hajajiunga na kikosi chake cha Liverpool kwa madai kuwa yupo majeruhi pia hataki kuendelea na kikosi hicho kwa kuwa anataka kujiunga na Barcelona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya michezo ya kalenda ya Fifa, hivyo amekutana na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Neymar ambaye aliitumikia Barcelona kwa misimu minne kabla ya Agosti 3, mwaka huu kujiunga na PSG kwa kitita cha pauni milioni 200, inadaiwa kuwa amemshauri asijiunge na Barcelona.

Naymar amemwambia Coutinho kuwa asijutie maamuzi ya klabu yake kukataa kumwacha akijiunga na kikosi cha Barcelona, ni bora aendelee kubaki Liverpool.

Kabla ya Neymar kujiunga na kikosi cha PSG, alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao wanamshawishi staa huyo wa Liverpool kujiunga na Barcelona ili wacheze pamoja, lakini baada ya Neymar kujiunga na PSG, kulikuwa na taarifa zingine kwamba mchezaji huyo anamshawishi ajiunge na klabu hiyo wawe wote.

Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thierry Henry, ametoa ushauri wa bure kwa Coutinho huku akimwambia kwamba ni vizuri akatumia njia sahihi ya kujiunga na Barcelona.

“Nitamshauri Coutinho kufuata njia sahihi ya kujiunga na Barcelona kama ilivyo kwa Luis Suarez, ni wazi kwamba anataka kuondoka kila mmoja anajua hilo, lakini kutokana na hali iliyopo ndani ya Liverpool, ni vizuri akaendelea kuwepo ndani ya klabu hiyo.

“Inawezekana msimu huu ukawa wa mafanikio makubwa ndani ya Liverpool, hivyo ni vizuri akamalizia msimu huu na kujiandaa na uhamisho wa msimu ujao. Coutinho ni miongoni mwa wachezaji ambao ninawakubali kutokana na uwezo wake.

“Endapo ataendelea kuwa kwenye kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp msimu huu, atazidi kujiongezea mashabiki wengi, bado anapendwa sana na Liverpool,” alisema Henry.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles