27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kupanda miti

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini watanzania wameshauriwa kupanda miti ya matunda na vivuli ili kulinda na kutunza mazingira.

Hayo yameelezwa leo,Desemba 23 mwaka huu  jijini Dodoma na Mtunza fedha wa kikundi cha kutunza na kuhifadhi mazingira cha  ‘Chapakazi’ Darwesh Saidi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Kikundi hicho cha Chapakazi  kinajishughulisha na uuzaji wa miche ya matunda na vivuli ambapo kinapatikana katika eneo la barabara ya Iringa Mkoani Dodoma.

Darwesh amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini watanzania wanatakiwa kupanda miti ya matunda na vivuli ili kuweza kutunza mazingira.

“Hapa kwetu kuna miche ya kila aina na tumekuwa tukiwapandia watu garden sasa huu ndio wakati wa kupanda miche ya kila aina ili iweze kuota vizuri lakini pia na kutunza mazingira,”amesema Darwesh.

Amesema katika kikundi chao,miche ya matunda inayopatikana ni pamoja na Miembe,Michungwa,Miparachichi na Milimao,

Ameitaja miche mingine iliyopo ni pamoja na  Miche ya kimvuli,ambayo ni  Mitimaji,Miarobaini,Mitingia na Codian,Miche mingine iliyopo  ni ya mbao ambayo ni Greveria, Mitiki,

Kwa upande wa maua amesema yaliyopo ni Biscas,Exola,Jesus,Lamanda,pamoja na Maua aina ya Parma ambayo ni  Royal Palm,Travell Parm na Golden Parm.

Darwesh pia amesema katika eneo lao hilo kunapatikana vyungu vya kila aina vikiwemo vinavyotengenezwa kwa vigae.

“Pia katika eneo hili watu wanapiga picha kwa ajili ya kumbukumbu pamoja na maharusi lakini tumekuwa tukitembelewa na wadau mbalimbali,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles