Serikali inatengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji

0
291

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara amesema Serikali inatengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji wanaofuata sheria.

Waitara ametoa kauli hiyo leo Desemba 23, 2020 alipotembelea kiwanda cha Saji Packaging kinachojihusisha na uzalishaji wa vifungashio vya plastiki na kurejeleza taka za plastiki kilichopo Iliemela jijini Mwanza.

Akionesha kuridhishwa na shughuli za kiwanda hicho alisema ni rafiki kwa mazingira kutokana na kukusanya taka za plastiki ambazo zingezagaa ovyo na kuzitumia kama malighafi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here