25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Uongozi yatakiwa kupika viongozi bila kujali tofauti

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi ameitaka Taasisi ya Uongozikuwaandaa Viongozi wa aina zote bila kujali tofauti zao ili waweze kutoamchango katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Uongozi (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Taasisi hiyo na kuhimiza uwajibikaji. Kulia kwake ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo.

Ndejembi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati waziara yake ya kikazi katika Taasisi ya Uongozi yenye lengo lakufahamiana na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa taasisi hiyo.

Ndejembi amesema Taasisi ya Uongozi ikijikita katika kuwaandaaviongozi bora itakuwa ni taasisi ya mfano na kuigwa Barani Afrika jamboambalo litaleta sifa nzuri kwa nchi yetu.

“Taasisi ya uongozi ikifanikiwa kuwaandaa viongozi bora nchini,itawawezesha Watanzania popote walipo kujivuna kwa kuwa na taasisiyenye mchango mkubwa wa kutoa mafunzo kwa watu waliopewamamlaka ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo,”amesema.

Aidha, Ndejembi amewahimiza watumishi wa Taasisi ya Uongozikuwa na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo iliiweze kufikia malengo iliyojiwekea.

Akiwasilisha utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo amesemataasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuandaa na kuendesha mafunzo yaviongozi, kuendesha majadiliano ya kisera na kufanya tafiti za kisera, kutoa ushauri wa kitalaam kuzisaidia taasisi na viongozi wakekutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Taasisi ya Uongozi ilianzishwa Julai, 2010 lengo likiwa ni kuwa na Kituocha utalaam wa juu cha kuendeleza Viongozi Barani Afrika kwa kuanziaTanzania, Kanda za Afrika Mashariki na hatimaye Afrika nzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles