31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya Barabara Pwani yaipigia chapuo Tarura kuongezwa bajeti

Na Gustaphu Haule, Pwani

Wajumbe wa bodi ya Barabara ya mkoa wa Pwani wamewapigia debe wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa kutaka waongezewe fedha zaidi ili waweze kutekeleza miradi yao kwa ufanisi zaidi.

Maazimio ya wajumbe hao yamekuja katika kikao cha bodi hiyo iliyofanyika jana Mjini Kibaha chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.

Katika kikao hicho ilibainika kuwa Tarura wanahudumia barabara nyingi zenye kilomita zaidi ya 5,000 huku wakipata fedha kutoka mfuko wa barabara asilimia 30 tofauti na Tanroads wanaopata aslimia 70.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Ramadhani Posi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze amesema Tarura wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa utengenezaji wa barabara kuliko Tanroads.

Amesema anashangaa kuona Tarura ambao wamekuwa wakihudumia barabara nyingi kila mwaka wakipewa bajeti ndogo huku Tanroads ambao wanafanyakazi katika barabara chache wakipewa fedha nyingi.

Posi,alisema Tarura wanapata bajeti ya asilimia 30 lakini Tanroads wanapata asilimia 70 jambo ambalo linapaswa kuangalia upya huku akipendekeza Tarura wapandishiwe mpaka asilimia 40 na Tanroads wapewe asilimia 60.

Nae mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo alisema ili barabara ziweze kupitika ni vyema Tarura wakapewa nguvu zaidi ya kifedha.

Mmoja wa wajumbe wa bodi ya barabara ya mkoa wa Pwani ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Michael Mwakamo akichangia mada katika kikao hicho kilichofanyika jana Mjini Kibaha. Picha na Gustaphu Haule

Alisema kuwa,fedha wanazopata hivi sasa hazitoshelezi kuzifanya barabara zote ziweze kufikiwa kwani wao ndio wenye majukumu makubwa ya kuhakikisha barabara wanazohudumia zinapitika muda wote.

“Mimi naunga mkono hoja zilizotolewa na wabunge wenzangu na wajumbe wengine wa bodi hii naomba Tarura waongezewa asilimia za fedha wanazopata kutoka asilimia 30 ya sasa mpaka kufikia asilimia 40,” alisema Mwakamo.

Mwakamo aliongeza kuwa kama Tarura watafanikiwa kuongezewa fedha hizo anaimani barabara zote za Mijini na Vijijini zinazosumbua zitakuwa zimepata usumbufu na hivyo kuzifanya ziweze kupitika wakati wote.

Kwa upande wake Mhandisi Ndikilo,ameunga mkono hoja hiyo ambapo aliwataka wabunge kwenda bungeni kwa ajili ya kuzisemea jambo hilo.

Aliisema Tarura ni chombo cha Serikali ambacho kilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha inatatua kero za barabara zilizopo Mijini na Vijijini lakini inakuwa jambo la ajabu kuona bado changamoto zinakuwa kubwa badala ya kupungua.

Alisema,wabunge ndio waanzilishi wa wakala huo kwahiyo bado wanayonafasi kubwa ya kulisemea jambo hilo ili ifike mahali wakala hao waweze kufanyakazi iliyokusudiwa na hivyo kuwasaidia wananchi kusafirisha bidhaa kwa haraka.

Aidha,Ndikilo amewaagiza watendaji wa Tarura kuonyesha jedwali la utengenezaji wa barabara zake na maeneo husika ya utekelezaji wa miradi hiyo ili kuleta ulinganifu na Tanroads na kwamba jambo hilo litakuwa rahisi kupitisha bajeti yao.

Hatahivyo,Ndikilo alisema ipo miradi mingi ya ujenzi wa barabara iliyoahidiwa na Rais Dk..John Magufuli ambapo aliwataka watendaji wa Tarura na Tanroads kuainisha ili ziweze kukumbushwa.

“Miradi yote ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami iliyoahidiwa na Rais Dkt.John Magufuli iwekeni pamoja ili tuweze kuifuatilia na miradi hii haina wasiwasi kwakuwa inajulikana,”alisema Mhandisi Ndikilo.

Hata hivyo, alitaja baadhi ya aadi hizo kuwa ni pamoja ni barabara ya Makofia-Mlandizi-Vikumburu mpaka Mzenga,Tamco -Vikawe pamoja na ile ya Utete -Nyamwage iliyopo Wilayani Rufiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles