30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Watakaouza mbolea chini ya kiwango kunyang’anywa leseni

Nora Damian, Dar es Salaam

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amewatahadharisha wasambazaji na wauzaji wa mbolea nchini kuzingatia ubora na watakaouza chini ya kiwango watanyang’anywa leseni na kufungiwa kufanya biashara kwa miaka mitatu.

Akizungumza leo Jumatano Februari 19, Hasunga ameziagiza mamlaka husika kuhakikisha zinafuatilia na kukagua kuangalia ubora wa mbolea zinazouzwa.

“Lazima tujiridhishe kwa sababu wachakachuaji wapo. Na ikionekana unauza mbolea ambazo zipo chini ya kiwango tutakunyang’anya leseni na kukuzuia kufanya biashara kwa miaka mitatu,” amesema.

Aidha, amezitaka kampuni zilizopewa kibali cha kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi kuingiza kiasi chochote wanachotaka lakini hazitaruhusiwa kuuzwa zaidi ya bei elekezi.

Kwa mujibu wa Hasunga mahitaji ya mbolea nchini ni tani 586,604 na hadi kufikia jana tani 491,659 ambazo ni asilimia 84 ya mahitaji zimeshaingizwa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles