28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi waichapa KMC wajituliza kileleni

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

YANGA imedhirisha kuwa msimu huu  wa Ligi Kuu Tanzania Bara  ina jambo lake baada ya kushinda mchezo wa tatu mfululizo kwa kuichapa KMC mabao 2-0  katika  mechi iliopigwa leo Oktoba 19, 2021 kwenye Uwanja wa Maji Maji, mjini Songea.

Mabao ya Wanajangwani hao yamefungwa na Fiston Mayele dakika ya tano na Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 12 na kuifanya Yanga kufikisha alama tisa na kukaa kileleni mwa ligi hiyo.

Fiston Mayele akimtoka beki wa KMC Andrew Vincent ‘Dante’ katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo kwenye dimba la Maji Maji, Songea.

Ushindi wa leo unaonesha muelekeo wa kufanikiwa kwa mipango ya  kocha wao Nasreddine Nabi  ambaye  kabla ya mchezo huo alisema mikakati yake ni kushinda bao zaidi ya moja tofauti na michezo miwili iliyopita ambayo wameshinda kwa bao moja moja,pia kulinda lango lao  wasiruhusu kufungwa.

Djuma Shaaban akichezea mpira katika mchezo huo

Mchezo wa kwanza msimu huu, Yanga ilicheza na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kisha kukutana na Geita Gold dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa upande wa KMC, kipigo cha leo kinaifanya kuendelea kuwa mkiani ikiwa na alama moja baada ya kucheza mechi tatu, ikipoteza mbili na kutoka sare moja.

Kikosi cha Wananchi kilichoanza leo dhidi ya KMC

Ikumbukwe  kuwa msimu uliopita Oktoba 25, 2020, KMC  ambayo pia leo ilikuwa mwenyeji, ilipeleka mchezo wake na  Yanga jijini Mwanza na kufungwa  mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles