25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yaungana na Boxer msibani

Na Mwandishi Wetu

KIKOSI cha Yanga kimerejea leo Oktoba 20, kutoka Songea na kuungana na mchezaji wao Paul Godfrey ‘Boxer’ kuaga mwili wa baba yake mzazi aliyefariki juzi kwenye hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.

Yanga imetua Dar ikitokea Songea katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini humo na Wanajangwani hao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Wachezaji wa Yanga wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa baba mzazi wa Paul Godfrey ‘Boxer’ katika Hospitali ya Temeke.

“Kwa niaba ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga, uongozi  wa Yanga unatoa pole kwa mchezaji wetu na familia yake yote kwa msiba huu mzito na kwamba klabu iko pamoja naye katika kipindi hiki cha majonzi.

“Mwenyezi Mungu aendelee kumpa nguvu mchezaji wet una familia yake kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu,” imeandika Yanga.

Viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wa Yanga wakiaga mwili Paul Godfrey ‘Boxer’

Baada ya kumaliza kuaga kikosi hicho kimeelekea moja kwa moja kambini, Avic Town, Kigamboni kujiandaa  wa Ligi Kuu dhidi ya Azam utakaopigwa Oktoba 30, 2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles