Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mashabiki wa Klabu ya Yanga waliojitikeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo Mei 28, 2023 kwa ajili ya kushuhudia mechi ya Fainali kombe la Shirikisho barani Afrika mkondo wa kwanza dhidi ya USM Alger ya Algeria wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa hamasa kubwa aliyoiweka kwenye michezo hadi wamefika hatua ya fainali.
Wakizungumza na Mtanzania Digital Uwanjani hapo mapema leo, mashabikia hao wamemhakikishia Rais Samia timu yao kuibuka na ushindi mnono katika mchozi huo wa kwanza wa hatua ya fainali.
“Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan anasapoti sana michezo nchini kwetu na kutokana na Yanga imeendelea kufanya vizuri kimataifa kwa kuwakilisha vyema nchi yetu Tanzania, hivyo niseme tu kwamba leo Mwarabu lazima afe bao tatu hapa kwa Mkapa na ytukienda kwake tunasuluhu ndoo lazima ije Tanzania, hivyo niseme tu kwamba wananchi tuko kamiligado leo,” amesema mmoja wa mashabiki hao.
Shabiki mwingine wa Yanga, Hamza Hassan, amemshukuru Rais Samia kwa mchango anaoutoa katika soka hapa nchini huku akumuomba mchango huo uende katika michezo mingine.
“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kununua tiketi ili tuweze kuingia bure kuisapoti timu yetu, nimuombe tu mheshimiwa rais mchango huu isiishie hapa,” amesema Hassan.
Mashabiki mbalimbali na wapenda michezo kwa ujumla wamejitokeza katika dimba la Benjamini mkapa huku wakiwa wamebeba mabango mbalimbali yenye ujumbe wa kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika sekta ya michezo.
Saa 10 jioni ya leo Yanga inashuka katika dimba la Benjamini Mkapa kwa ajili ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika mkondo wa kwanza dhidi ya USM Alger ya Algeria, huku mchezo wa pili ukitarajiwa kupigwa Juni 3, nchini Algeria.
Mtanzania Digita tunasema kila la heri Yanga mkapeperushe vema bendera ya Taifa letu Tanzania.