26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo: Watanzania wanamnyima usingizi Rais Samia

Na Raymond Minja, Iringa

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema matamanio ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuona changamoto za wananchi kwenye maeneo yao zinatatuliwa na kuleta matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.

Chongolo ametoa kauli hiyo wilayani Mufindi Mei 28, wakati wa muendelezo wa ziara yake ya siku saba mkoani Iringa yenye lengo la kukagua uhai wa CCM na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya 2020-2025.

“Mwenyekiti wa CCM ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan halali usingizi kutokana na changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa ili nchi iweze kupiga hatua katika maendeleo,” amesema Chongolo.

Amesema kwa sababu ya dhamira njema kwa Watanzania ambayo inaoneshwa na Rais Samia ya kuhakikisha matokeo chanya yanaonekana, amewataka viongozi wilayani Mufindi kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza wananchi na kutatua changamoto zinazowakabili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles