Na TIGANYA VINCENT-TABORA
Agizo hilo limetolewa jana wilayani Tabora na , wakati alipotembelea Shule ya Sekondari Tabora ili kujionea maendeleo ya ukarabati chini ya utaratibu wa ukarabati wa shule kongwe nchini.
Katika maelezo yake, Manyanya aliwaambia wanafunzi hao kuwa wanafunzi wote nchini wanatakiwa kufuata sheria za shule na za nchi ili wamalize masomo yao bila kupata matatizo ikiwamo kufikishwa mahakamani.
“Mnatakiwa kufuata sheria na taratibu za shule kama mlivyoelekezwa. Mkitoroka shule na kwenda mitaani na kufanya fujo, mtashughulikiwa kwa sababu mtakuwa mmevunja sheria,” alisema Manyanya.
Katika hatua nyingine, naibu waziri huyo aliwataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora, kuepuka kujiingiza katika vitendo vitakavyokatisha ndoto zao kwa sababu ya kupata ujauzito.
Alisema ni vema wasome kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza kukatisha ndoto zao kwani jamii na Taifa linawategemea katika kushika nafasi mbalimbali.
Pia, aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wawe tayari kukabiliana na ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Akitoa taarifa ya ukarabati unaoendelea, Mkuu wa Shule ya Sekondari Tabora, Marwa Robert, alisema ukarabati unaendelea vizuri na zimebaki siku 60 ili mjenzi akabidhi kazi.
“Ukarabati unakwenda vizuri na utagharimu shilingi milioni 999. Hadi sasa kazi zilizofanyika ni pamoja na kubomoa na kuziba nyufa, kupaka rangi, ukarabati wa madirisha, milango, kurejesha vyoo, ukarabati wa maktaba ya zamani, ujenzi wa maktaba mpya na kuandaa miundombinu ya maji