27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 90,7802 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza

Na Mwandishi Wetu

JUMLA ya Wanafunzi 907,802 waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba mwaka huu wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza ,kati yao wasichana 467,967 na wavulana  439,835 sawa na asilimia 81.9 ya wanafunzi waliofanya  mtihani wakuhitimu elimu ya  shule ya msingi mwaka 2021.

Hayo yameelezwa jana Novemba 24,2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Waziri Ummy amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2022.

Amesema zoezi hilo limehusisha jumla ya wanafunzi 907,802 wakiwamo wasichana 467,967 na wavulana 439,835 ambao ni sawa na asilimia 81.97 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2021.

Amesema kati ya waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,673 sawa na asilimia 0.29 ambao kati yao wavulana ni 1,471 na wasichana 1,202.

Aidha kwa mwaka 2022 ongezeko la wanafunzi waliofaulu ni wanafunzi 73,932 sawa na ongezeko la  asilimia 8.87 la wanafunzi waliofaulu tofauti na mwaka 2020 walikuwa 833,872 ambapo kati ya wanafunzi hao wapo  wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,673 sawa na asilimia 0.29 kati yao wavulana 1,471 na wasicha 1,202.

Amesema kwa mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 73,932 sawa na asilimia 8.87 ya wanafunzi waliofaulu ukilinganisha na mwaka, 2020 ambapo jumla ya wanafunzi 833,872 walifaulu na kupata sifa ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza.

Mfumo kielektroniki ulivyorahisisha uchaguzi wa wanafunzi

 “Mwaka huu kwa mara ya pili uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza umefanyika kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Uchaguzi wa Wanafunzi (Students Selection-Management Information System),”amesema.

Waziri Ummy amesema mfumo huo umesaidia kupunguza muda unaotumika kwenye uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza,kupunguza gharama zinazotumika wakati wa zoezi la uchaguzi na upangaji wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza.

Amesema pia mfumo huo umesaidia kuongeza ufanisi na uwazi katika uchaguzi wa wanafunzi kwa maana ya kuwa kila mwanafunzi anapangwa kwenye shule kulingana na mwongozo wa uchaguzi unavyoelekeza.

Ataja siku ya kuanza masomo

Waziri huyo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI ilifanya maandalizi mapema kuhakikisha kuwa wanafunzi wote watakaofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2021 wanajiunga na Elimu ya Sekondari ifikapo Januari, 2022.

Amesema kutokana na maandalizi hayo wanafunzi wote 907,802 waliofaulu mtihani wa darasa la saba nchini mwaka 2021 wataanza masomo yao siku moja mara muhula wa masomo utakapoanza.

“Na katika hatua hii natangaza kuwa muhula wa masomo kwa Shule za Msingi na Sekondari zinazomilikiwa na Serikali kwa mwaka 2022 utaanza tarehe 17 Januari 2022,” amesema.

Amshukuru Rais Samia

Pia Waziri Ummy amemshukuru Rais Samia kwa kutilia mkazo suala la elimu ya sekondari, na kwa mara ya kwanza aliruhusu jumla ya shilingi bilioni 240 kutumika kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 12,000 nchi nzima.

Amesema kabla ya uamuzi wa Rais Samia kuongeza vyumba vya madarasa 12,000, shule za serikali za umma zilikuwa na nafasi 430,604 kwa ajili ya kidato cha kwanza ambazo zinaachwa na wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne mwaka 2021.

“Ujenzi huu wa vyumba vipya vya madarasa 12,000 utawezesha upatikanaji wa nafasi za nyongeza 600,000 na hivyo kuwa na jumla ya nafasi 1,030,604 kwa ajili ya kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2022 na hii inaleta ziada ya nafasi 122,802 za kidato cha kwanza kulinganisha na wanafunzi waliofaulu ambao ni 907,802,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles