24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Homa yazidi kupanda washiriki Miss E.A

Na Beatrice Kaiza,Mtanzania Digital

MAANDALIZI ya shindano la urembo la Afrika Mashariki ‘Miss East Africa 2021’, yamefikia patamu ambapo washiriki  wanatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtanzania Digital,

Makamu wa Rais wa mashindano hayo, Jolly Mutesi, amesema washiriki wapo tayari kwa maandalizi ya mwisho, huku fainali ikitarajia kufanyika Desemba 17, 2021 kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Amezitaja nchi shiriki katika shindano hilo kuwa ni mwenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, South Sudan na Somalia, Reunion, Ethiopia, Malawi, Burundi na Mauritius.

“Tanzania itawakilishwa na mrembo Queen Mugesi ambae aliwashinda warembo zaidi ya 2,600 wa Tanzania walioomba kuiwakilisha nchi kwa njia ya mtandao.

“Queen alichaguliwa katika mchakato ulioendeshwa na wataalamu wa mambo ya urembo kwa zaidi ya mwezi mmoja,” amesema.

Amefafanua kuwa mashindano ya ‘Miss East Africa’ yanayoandaliwa na kampuni ya Rena Events, yaliasisiwa na Mtanzania Rena Callist mwaka 1996, yanatarajiwa kuangaliwa na zaidi ya watu milioni 200.

Amesema kiingilio cha chini katika fainali ya kumpanda mrembo wa Afrika Mashariki kuwa ni sh 50,000 kwa tiketi za kawaida na sh 100,000 VIP na sh 200,000 kwa VVIP.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles