31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Nissan Navara kuleta mapinduzi Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya magari ya Nissan Tanzania imetambulisha gari jipya  aina ya  Nissan Navara ikisema limekuja kuleta mapinduzi katika sekta ya usafirishaji Afrika.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa gari hilo uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Vingunguti, Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Alfred Minja, amesema gari hilo limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu.

“Nissan Navara ni toleo la 2021 ni gari ambayo inaweza kwenda katika sehemu yoyote Tanzania na inaweza kufanya kazi katika sekta zote, ina uwezo wa kubeba kilo 1,054 na kuvuta mzigo wa kilo 750,” amesema Minja.

Amesema pia ukubwa wa tanki la mafuta ni lita 80 ambazo zinaweza kutumika kwa zaidi ya kilomita 1,000 na kwamba bei yake ni Dola za Marekani 53,800 sawa na Sh milioni 124.2.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Nissan katika nchi za Jangwa la Sahara, Tim Jacques, akizungumza wakati wa kutambulisha gari jipya aina ya Navara. (Wapili Kushoto) ni Mkurugenzi wa Nissan Tanzania, Christophe Henning, Meneja Masoko na Mauzo, Alfred Minja naMeneja Ufundi wa kampuni hiyo, Samir Baksh.

Naye Mwenyekiti wa Nissan katika nchi za Jangwa la Sahara Tim Jacques, amesema wataendelea kubuni magari mbalimbali yenye ubora wa hali ya juu ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo Navara ilianza kutambulishwa Afrika Kusini ikafuatiwa na Kenya, Zambia kisha hapa nchini.

Meneja Ufundi wa kampuni hiyo, Samir Baksh, amesema gari hilo ambalo linatumika njia zote lina mifumo mingi na ikitokea breki za ghafla ina uwezo wa kukamata na kuendelea na safari.

Aidha amesema baada ya kutembea kilomita 10,000 gari hilo hufanyiwa ‘service’ bure.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Nissan Tanzania, Christophe Henning, amesema uwepo wa kampuni hiyo nchini umetoa fursa za ajira kwa Watanzania.

Aidha amesema kupitia sera yao ya kusaidia jamii wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwa jamii kama vile vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona na vifaa vya kujifunzia katika Shule ya Viziwi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles