25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Walinzi kizimbani kwa wizi

Na AVELINE KITOMARY DAR ES SALAAM

WALINZI wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni   Dar es Salaam, wakikabiliwa na  mashtaka matatu ya kula njama, kutenda kosa la wizi, kushindwa kuzuia uhalifu na wizi wa gari.

Waliopandishwa kizimbani ni Julius Lamyaki (24) mkazi wa Madale na Yohana Salim (25) mkazi wa Kulangwa.  

Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Abudi Yusuph alidai mbele ya Hakimu Anifa Mwingira kuwa katika tarehe isiyojulikana Machi mwaka huu eneo la Goba Kulangwa, Wilaya ya Kinondoni walikula njama kutenda kosa la wizi.

Shtaka la pili watuhumiwa wanadaiwa   Machi 17 mwaka huu eneo la Goba Kulangwa Wilaya ya Kinondoni, waliiba gari l namba   T.643 DME aina ya Mitsubishi Canter yenye thamani ya Sh milioni 34 mali ya Ephrahim Malile.

Katika shtaka la tatu washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa   Machi 17 mwaka huu eneo la Goba Kulangwa kama walinzi katika duka la vifaa vya ujenzi la Chelestino Malile walishindwa kuzuia uhalifu. Washtakiwa wote walikana mashitaka  na walirudishwa rumande hadi Mei 9 mwaka huu kesi itakapotajwa tena. Wakati huo huo, mahakama imempandisha kizimbani David Yambesi (33) mkazi wa Goba kwa mashtaka matatu ikiwamo kujipatia mali ya udanganyifu.

Akisoma  shtaka hilo mbele ya Hakimu Anifa Mwingira, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri Matarasa Hamisi  alidai katika shtaka la kwanza    Julai 4 mwaka 2017 Wilaya ya Kinondoni  mshatakiwa alionyesha hati ya kugushia ya mauzo ya gari   ya Toyota SWIFT  namba   T.452 DGW mali ya Sophia Nyangasha.  Katika shtaka la pili, mshtakiwa alidaiwa   Julai 04, 2017 katika ofisi za TRA Mwenge Wilaya ya Kinondoni alionyesha nyaraka za uongo  kwa ofisa wa TRA kwa lengo la kudanganya kuwa yeye ni mmiliki wa gari hilo. 

Shtaka la tatu mshatakiwa   Juni 28 mwaka jana katika ofisi za Platinum Credit LTD Wilaya ya Kinondoni, kwa udanganyifu alijipatia   Sh millioni tatu kinyume cha sheria.  

Mshtakiwa alikana mashitaka na alirudishwa rumande hadi Mei 13 mwaka huu, kesi itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles