23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Trafiki wakusanya Sh bilioni 10.8 kwa miezi 27

Na ELIYA MBONEA -ARUSHA KIKOSI cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, kimekusanya Sh 10.864,170,000 za faini kutoka kwenye makosa 362,136 kwa kipindi cha Januari 2017 hadi Machi 2019.

Akitoa taarifa  ya kikosi hicho, RTO Joseph Bukombe, alimuomba Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana, awaunge mkono kuhakikisha deni la Serikali Sh bilioni 13 zilizopo nje zinakusanywa.

Bukombe alisema  kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu hakuna ongezeko la ajali za barabarani.  Akizungumzia wiki ya nenda kwa usalama, alisema, “mpaka sasa magari ya watu binafsi na ya biashara 17,000 na pikipiki 5,000 yamekaguliwa.

Hatua hii itadumu kwa miezi mitatu baada ya hapo utakuwa ukaguzi wa lazima. “Hatua inafanyika chini ya kaulimbiu ya “Paza Sauti”, kila anayetumia chombo cha moto barabarani akiona hatari ya kusababisha mtu kujeruhiwa au kupata madhara anatakiwa kutoa taarifa.

“Tunaamini kila mtu akipaza sauti kwa kusaidia muhusika alazimishwe kutii sheria hakutakuwa na madhara na hapo tutaokoa maisha ya watu,” alisema RTO Bukombe. Kuhusu hali ya usalama kwa January hadi Machi mwaka huu alisema   ajali 10 zilitokea ambako ajali za vifo zilikuwa saba, waliokufa watu tisa, ajali za majeruhi tatu, waliojeruhiwa watu 17.

Alisema kwa Januari hadi Machi mwaka 2018 ajali zilikuwa 15 ambako ajali za vifo 11, waliokufa 12, ajali za majeruhi tatu, waliojeruhiwa 14 na ajali ya kawaida moja. Alisema kikosi hicho kimeongeza juhudi za kukamata makosa hatarishi   kukabiliana na ajali za barabarani, ikiwamo kuongeza doria kwa kutumia Speed Radar.

“Tumejizatiti maeneo hatarishi kwa kuhakikisha madereva wanafuata sheria hasa yenye miteremko mikali na makazi ya watu. “Lakini pia upimaji wa ulevi kwa madereva nazo zimeendelea kufanyika maeneo mbalimbali hasa kituo na kuwabaini madereva. “Ukiruhusu makosa madogo ya barabarani utakuwa unakaribisha makosa makubwa na madhara zaidi kwa watu,” alisema RTO Bukombe.

Alitumia fursa hiyo kuwataka wanaodaiwa na Serikali kulipa madeni yao kwa sababu  yeyote anayedaiwa hatatoka salama mkoani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles