24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mnada wa kokoa kuanzishwa Kyela

Arodia Peter, Dodoma

Serikali imesema itaanzisha mnada wa kuuza zao la kokoa linalozalishwa Kyela mkoani Mbeya.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda, Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa bungeni leo Aprili 30, amesema mkakati wa Serikali ni kutafuta wanunuzi wakubwa duniani kununua mazao kwenye mnada huo na kuachana na ule wa Mombasa nchini Kenya.

Awali Bashungwa pia ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa pamba ambao wameanza kununua zao hilo kabla ya msimu kuanza Mei mwaka huu.

Akijibu swali la Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa kuhusu  nini kauli ya Serikali kwa wafanyabiashara walioanza kununua pamba kwa Sh 600 na 700.

Bashungwa amesema: “Anayenunua pamba kabla ya msimu kuanza rasmi ni kosa kisheria na atawasiliana na Wakuu wa Mikoa washughulikie suala hilo,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles