27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa miwa Kilombero wamkosoa Mpina

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakulima wa Miwa katika Bonde la Mto Kilombero mkoani Morogoro wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na baadhi watu waliodanganya kuwa ni wawakilishi wa wakulima na kudai bei ya miwa imeporomoka na hawalipwi fedha zao kwa wakati.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 31,2024 Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Ushirika Bonde la Kilmbero, Bakari Kangamo, amesema wao pamoja na baadhi ya wakulima wanaounda vyama 17 vya ushirika (AMCOS), wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa ni uzushi na upotoshaji unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa.

“Hakujawahi kutokea bei ya miwa kushuka kwani tangu tuanze kuuza miwa msimu huu tumeuza kwa bei ya laki moja na elfu nane (108,000) – tofauti na hizi taarifa za uongo zinazosambaa,” amesema Bakari Kangamo, mmoja wa wakulima hao.

Aidha, wakulima hao wamedai kuwa hakujawahi tutokea ucheleweshwaji wa muda mrefu wa malipo kwa wakulima kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha miwa na badala yake malipo yalichelewa kwa siku mbili tu kutokana na mifumo mipya iliyowekwa kiwandani hapo ambapo walitakiwa kulipwa tarehe 15 na badala yake walilipwa tarehe 17.

Wakulima hao wamesisitiza kwamba hakuna athari zozote zilizowapata kufuatia uamuzi wa serikali kutoa vibali vya kuagiza sukari nje kupunguza ongozeko la bei ya bidhaa hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Vilevile wakulima hao wamesema kuwa vyama vyao vina ushirikiano mzuri na kiwanda cha sukari Kilombero na wanayo matumaini makubwa ya mageuzi ya zao hilo, kwa kuwa kiwanda hicho kinalenga kufanya upanuzi mkubwa utakaopelekea wakulima kuuza miwa kwa wingi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles