29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wakandarasi wa miradi ya maji waonywa kufanya kazi kwa mazoea

Na Amina Omari, Pangani

Serikali imewataka wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa miradi ya maji nchini kuacha siasa na kufanyakazi kwa mazoea.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa maji, Mhandisi Marry Prisca Mahundi wakati akiongea na wananchi wa kata ya Sakura wilayani Pangani mkoani Tanga akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo.

Amewataka Wataalamu hao kuacha kufanyakazi kimazoea kwani wanakwamisha malengo ya serikali ya kuharakisha kuwapelekea maendeleo wananchi wake.

“Wakandarasi achane kufanyakazi kwa mazoea kwenye sekta ya maji tunataka matokeo bora na ya haraka ni wananchi kupata maji Safi na salama ya uhakika,” amesema Mahundi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jumuiya ya watumia maji Sakura (SIBIUSO), Yusuf Ramadhani amesema mradi wa maji wa Kwakibuyu unahudumia wakazi 7780 kwa sasa ukiwa na vituo 27 vya kuchotea maji.

“Tunaiomba serikali itusaidie kukarabati miundombinu ya mradi kwa imechakaa ni ya muda mrefu na inasababisha wakati mwingine upungufu wa maji katika baadhi ya vituo” amesema Ramadhani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles