29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Msimu wa kwanza wa Runway bay wazinduliwa Zanzibar

Na Jeremia Ernest

Msimu wa kwanza wa Tamasha la Mitindo la ‘Runuway bay’ umezinduliwa jana katika hotel ya Kendwa Rocks kisiwani Zanzibar.

Wabunifu watano walionyesha mavazi yao kupitia wanamitindo wakongwe na chipukizi kutoka kisiwani Zanzibar na Bara pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mahiri akiwemo Beauty na Steven Maduro.

Akizungumza na wandishi wa habari katika uzinduzi huo Mratibu wa Tamasha hilo, Waiz Designer, aliwashukuru wadau na wana tasnia waliojitokeza pamoja na kuahidi burudani katika siku zilizobaki.

“Ninafuraha kwa kufika siku ya leo, napenda kuwakaribisha wageni wetu katika ‘Runuway bay’ tutakuwa na maonyesho haya kwa muda wa siku mbili kuachia leo,” anasema Waiz Designer.

Aliongeza kuwa: “Siku ya leo wanafanya maonyesho hayo katika eneo la Mizingani Sea front, jioni na kesho (leo) watahitimisha The Loop hoteli pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

Wabunifu waliopamba jukwaa hilo siku ya jana ni mama wa mitindo, Asia Idarus, Shey Collection, Dulla Teylor, Enjimaasai, Neh Collection, na Waiz Designer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles