New Delhi, India
Waziri wa mambo nje Nchini India Subramanyan Jaishankar amethibisha kuwa wajumbe wanaohudhuria mkutano wa G7 jijini London wakutwa na maambukizi ya Virusi vya corona.
Waziri Jaishankar ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii “Twitter” na kuongezea kuwa wajumbe hao kwa sasa wamejitenga na watahudhuria mkutano huo kupitia mtandao.
Afisa wa serikali ya Uingereza alisema washiriki wawili walipimwa na kupatikana na Corona baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kila siku katika mkutano huo.
Mkutano huo wa mataifa ya G-7 unaingia siku yake ya mwisho huku mawaziri wa Mambo ya nje wa mataifa hayo wakijadili usambazaji wa chanjo ya corona ulimwenguni.
Shirika la Afya Duniani WHO lilikuwa limehimiza mataifa yalioendelea kusaidia nchi masikini kupata chanjo hizo.