28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Mikoa na Wilaya endeleeni kuchapa kazi- Ummy

Nteghenjwa Hosseah, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Tawala za Mikoa Mhe.Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuchapa kazi kama awali na sio kukaa kusubiria uteuzi.

Waziri Ummy ameyasema hayo katika ziara yake Wilayani Chemba mkoani Dodoma wakati akikukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na Kamati ya Fedha pamoja na Menejimenti ya Halmashauri hiyo Mei 4, 2021.

“Hali inayoendelea kwa viongozi hawa haileti Afya, wengine hawafanyi kazi eti wanasubiria mkeka, hamuoni kuwa mnaonea wananchi kupata haki yao ya msingi ya kuhudumiwa,” alihoji Waziri Ummy.

Kipindi hiki mnatakiwa kuendelea kuchapa kazi kama kawaida kwani wananchi wanahitaji kuendelea kuhudumiwa, suala la mkeka unakuja lini hilo ni kuliacha kwa Mamlaka, ninyi chapeni kazi,” aliongeza Ummy

Aidha, Ummy aliwakumbusha viongozi hao kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku wakimtanguliza Mungu mbele ambaye ni mpangaji wa kila jambo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles