26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wajawazito wasisitizwa kutumia vidonge vya kuongeza damu

Na Yohana Paul, Geita

Kina Mama wajawazito na wale wenye mipango ya kupata watoto wameshauriwa kuwekea mkazo utumiaji wa vidonge vya kuongeza damu vinavyofahamika kama ‘Follic acid’ ili kuhakikisha mzunguko wa  damu mwilini ubakidhi  mahitaji ya mtoto tumboni katika hatua zote za  ukuaji.

Ushauri huo  ulitolewa hivi karibuni  na Muuguzi na Mkunga kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Grace Msemwa wakati akizungumza na MtanzaniaDigital hili kuelezea mambo ya msingi wanayopaswa kuzingatia kina mama wajawajizito ili kuweka mazingira rafiki ya ukuaji wa mtoto kwa kipindi chote cha ujauzito.

Grace alisema mama anapokuwa mjamzito mahitaji ya mzunguko wa damu yanakuwa makubwa mwilini hivyo ili mama na mtoto aliyepo tumboni wote wapate damu kwa kiwango sahihi ni lazima kuwepo na damu ya kutosha ambayo itaweza kufika kila sehemu pasipo changamoto yoyote na ndiyo maana ni muhimu kwa mjamzito kutumia vidonge vya kuongeza damu.

Alisema upatikanaji wa damu ya kutosha kwa mtoto aliyepo tumboni itasaidia kumkinga na magonjwa kama vile mgongo wazi na kichwa kikubwa ama kichwa maji na ndiyo maana mjamzito anashauriwa kutumia vidonge hivo ili kumkinga mtoto na ulemavu huo ambao unazuilika.

“Mbali na kwamba vidonge hivi ni muhimu zaidi kwa wajawazito lakini niwakumbushe pia vinaweza kutumiwa hata na mabinti ambao wameshafikia hatua ya kubeba ujauzito ambao wanaweza kuanza kutumia ili kutengeneza mazingira rafiki pale watakapopata ujauzito ila kwa mama mjamzito anatakiwa atumie pia hata atakappjifungua.

“Niwakumbushe pia wajawazito kuendelea kuhudhuria na kufuata maelekezo ya kliniki na pale wanapokutana na dalili hatarishi kama kichwa kuuma sana, kutokwa na damu ukeni, mtoto kucheza sana au kutokucheza, miguu kuvimba ni vyema wakawahi zahanati ama kituo cha afya kwa msaada zaidi kuepuka madhara  zinazoweza kumkuta mtoto au mama,” alisema Grace.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles