Na Asha Kigundula, Dar es Salaam
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Behnam Paul “Ben Pol” anatarajia kuuaga mwaka 2020 na kuukaribisha mwaka 2021 kwa staili ya kipekee kwa kujumuika na mashabiki zake.
Ben Pol anatarajia kufanya show kubwa ya Muziki wa Live na chakula cha jioni pamoja na mashabiki wake.
Akizungumza na MtanzaniaDigital leo Desemba 28, Ben Pol amesema Shoo hiyo inatarajiwa kufanyika Ramada Hotel, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam katika mkesha wa mwaka mpya Desemba 31, 2020 ambapo ataanza kwa kujumuika katika chakula cha jioni pamoja na mashabiki zake watakaohudhuria usiku huo.
Ben Pol amesema, pia kutakuwa na michezo ya watoto, urushaji wa fataki pamoja na muziki wa live ukiongozwa na Ben Pol na bendi yake.
“Mashabiki zangu wamekuwa wakizipokea vizuri sana kazi zangu kwa zaidi ya miaka 10 sasa, nashukuru kwa upendo na sapoti kubwa wanayonipa, nina kila sababu ya kusherehekea kwa kujumuika nao kwa chakula na muziki mzuri wa live kwenye mkesha wa mwaka mpya.
“Lakini pia hii haitoishia hapa, nitazunguka mikoani kufanya kitu kama hiki naomba nao pia wajiandae kunipokea tukijaaliwa uzima,” ameenda Ben Pol
Ben Pol kwa sasa anatamba na Wimbo wa Kidani aliomshirikisha mkwe Anerlisa kwenye video.