24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

WAFUGAJI WA KUKU WAPIGWA MSASA

Na FLORENCE SANAWA-MTWARA


ZAIDI ya vikundi 30 kutoka katika kata tano za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara vimetakiwa kuacha ufugaji wa kuku wa kienyeji bila kufuata kanuni za ufugaji.

Badala yake, wafugaji hao wametakiwa kuanza kufuga kisasa zaidi na katika mazingira bora, ili kuondokana na ufugaji wa mazoea.

Mafunzo hayo yametolewa mwishoni mwa wiki na Shirika Lisilo la Serikali liitwalo Society Against Poverty (MSOAPO), baada ya kufanya tafiti mbalimbali kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wananchi kiuchumi katika ufugaji wa kuku na nyuki.

Akizungumzia baada ya kupata mafunzo hayo, Asha Salum, kutoka Kijiji cha Mtandi, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, alisema mafunzo hayo ni chachu kwao katika uboreshaji wa ufugaji wa kuku.

“Awali tulikuwa tukifuga kuku huku tukiwa tunaishi nao ndani, hali ambayo ilikuwa inakwamisha watu wengi kukuza uchumi wao kupitia mifugo hiyo, kutokana na kushambuliwa na magonjwa kwa wakati mmoja,” alisema Salum.

Naye Asthma Ismail, mkazi wa Kijiji cha Madimba, alisema mafunzo hayo yamemsaidia na kumjengea uelewa zaidi juu ya ufugaji wa kuku, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo walikuwa wakiendesha maisha yake.

Naye Mohamed Picha, mkazi wa Kijiji cha Namayakata, alisema kama vikundi vyote vitazingatia maelekezo waliyopata, watapiga hatua kimaisha kwakuwa walikuwa hawajui namna ya kuwatunza na kuwadhibiti kuku.

“Sasa najua kuku yupi anataga yupi anakaribia kupata vifaranga na hii itatusaidia sisi kuandaa mabanda na tutakuwa na uwezo mkubwa wa kutunza vifaranga vya kuku ambavyo vitatusaidia kuongeza kipato,” alisema.

Naye Mratibu wa MSOAPO, Mustapha Kwiyunga, alisema hadi sasa wametoa mafunzo kwa vikundi 30 vinavyojishughulisha na ufugaji wa kuku katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles