22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

BEI ELEKEZI YA PAMBA YATAJWA

Na MWANDISHI WETU


WAZIRI wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba ametangaza bei elekezi ya kununulia pamba na mbegu msimu huu wa 2018/19 kuwa ni Sh 1,100 kwa kilo.

Akizungumza katika siku ya ufunguzi wa msimu wa ununuzi wilayani Igunga mwishoni mwa wiki, Dk. Tizeba alisema   bei hiyo imepatikana baada ya wadau kukubaliana.

 “Msimu huu bei ya pamba itakuwa Sh 1,100 kwa kilo moja kutokana na bei katika soko la dunia kuwa hairidhishi.

“Bado pamba yetu nyingi inauzwa nje ikiwa ghafi hali inayotufanya tuwe tegemezi kwenye suala la bei, lakini Serikali iko katika mchakato wa kuhamasisha maendeleo ya viwanda vya nguo nchini hali hii itaboresha bei ya pamba nchini,” alisema Dk Tzeba.

Dk. Tzeba alisema ili kumpunguzia mkulima mzigo wa madeni ya pembejeo na makali ya bei kushuka kwa Sh 100 kutoka ile ya msimu uliopita, Serikali imeamua kulibeba deni la zaidi ya Sh bilioni 30 la viuadudu ambavyo wakulima walikopeshwa msimu huu    waweze kunufaika na kilimo chao.

Alisema kuanzia msimu ujao wa kilimo, wakulima watapatiwa pembejeo zote ambazo ni mbegu, kamba za kupandia na viuadudu bure bila kulipia gharama yoyote.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Marco Mtunga alisema bei elekezi ya pamba inasimamiwa kwa Sheria Na.2 ya mwaka 2001.

Sheria hiyo  inaelekeza kwamba kabla ya msimu wa ununuzi wa pamba kuanza lazima wadau wa msingi wa zao hilo wakutane na kukubaliana juu ya bei.

Mtunga alisema pamba yote ya wakulima itanunuliwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS).

Alisema wakuu wa mikoa, wilaya, vyama vya ushirika na mrajisi wa ushirika wanawajibika kusimamia ununuzi na kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles