27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

LUKUVI APIGIA CHAPUO KODI ZA NYUMBA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa rai  kwa wadau wa nyumba kulipa kodi halali katika uendeshaji wa shughuli zao ili kwenda sawa na kasi ya ukuaji  uchumi kupitia mapato ya ndani.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki katika maonyesho ya milki kuu, nyumba na nyezo  yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge jijini hapa.

Maonyesho hayo yaliandaliwa na kampuni ya Terranova ya   Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali walijitokeza kuonyesha bidhaa mbalimbali katika sekta hiyo wakiwamo  Nabaki Afrika, Fumba Developments,  Ngorongoro Conservativation, Alrais Developers na Taasisi ya Mwanamke Ardhi.

Waziri Lukuvi alisema wadau wa nyumba wanatakiwa kulipa kodi halali katika uendeshaji wa shughuli zao   kwenda sawa na kasi ya ukuaji  uchumi kupitia mapato ya ndani.

“Rai yangu  kwa wadau wa nyumba ni kulipa kodi halali katika uendeshaji wa shughuli zao   kwenda sawa na kasi ya ukuaji  uchumi kupitia mapato ya ndani,” alisema.

Aliupongeza uongozi wa kampuni ya hiyo ya  wazalendo inayoongozwa na vijana waliopata   elimu katika vyuo vikuu vya    nchini, kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na masuala mbalimbali yakiwamo ya ardhi.

“Pamoja na ubunifu huo  wa waandaji uliolenga kuwafikia watanzania wote kwa wakati mfupi kupitia wawakilishi wao, hatua hiyo itasaidia kufikisha elimu kuhusiana na sekta nzima ya ardhi na kuiletea Tanzania mendeleo makubwa kutokana na rasilimali hii,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Terranova, Emil Sylvester, alisema wataendelea kuhamasisha wawekezaji wafike Dodoma kwa ajili ya kuwekeza.

“Sisi tumeanza na tutazidi kuhamasisha wawekezaji wafike Dodoma , ili azma kuu ya serikali ya kuhamia makao makuu ya nchi izidi kupata tija kwa maendeleo yetu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles