27 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji Simba wakutana na Rais Zanziba

Na Mwandishi Wetu

Wachezaji wa timu ya Simba, viongozi na benchi la ufundi wamekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 25,2024 baada ya kuwasili visiwani humo kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Azam utakaochezwa Uwanja wa Amani Complex.

Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar, Simba wamemkabi zawadi ya jezi Rais Dk. Mwinyi pamoja na mke wake mama Mariam Mwinyi.

Akizungumzia katika hafla hiyo, Rais Mwinyi ameipongeza kutokana na kuiwakilisha vyema kimataifa kwani jambo hilo linasaidia kukuza utalii kupitia michezo.

Pia Rais huyo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Sinajipanga kujenga uwanja mkubwa wa michezo utakaokuwa na vigezo vinavyokubalika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) pamoja na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha michuano ya soka inayowashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) na ile ya michuano ya soka ya mataifa ya Afrika kwa timu za taifa (AFCON), kuwa Zanzibar ni sehemu itakayochezwa michezo hiyo.

Pia Rais Dk. Mwinyi ameelezea dhamira ya Simba ya kujenga kituo cha kuwaendeleza vijana katika mchezo wa soka hapa Zanzibar (soccer academy) kuwa ni jambo jema na kuwaahidi Serikali ipo tayari kuwaunga mkono kwa kuwapa eneo la ujenzi wa kituo hicho.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha michuano ya soka inayowashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) na ile ya michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika kwa timu za Taifa (AFCON), kuwa Zanzibar ni sehemu itakayochezwa michezo hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amemhakikishia Rais Dk. Mwinyi kwamba klabu hiyo ipo tayari kuitangaza Zanzibar kimataifa kupitia utalii wa michezo.

Vilevile, amepongeza juhudi za Rais Mwinyi kuendeleza viwanja vya michezo kila wilaya Unguja na Pemba, kwani michezo ni nyezo muhimu ya kukuza umoja, furaha na upendo miongoni mwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles