27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wacheza Gofu 12 kuiwakilisha Tanzania ‘ European Tour Challenge’

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

JUMLA ya wachezaji 152 wa gofu wa kulipwa kutoka Mataifa mbalimbali ikiwamo Watanzania 12 ,wanatarajiwa kuchuana katika shindano la gofu lililopewa jina la ‘ European Tour Challenge litakalofanyika Aprili 7-10, 2022 kwenye viwanja vya klabu ya Kilimanjaro Golf Estate, jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 22, 2022 katika klabu ya Gofu Lugalo, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania(TGU), Chriss Martin, amesema ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya shindano hilo kubwa .

Martin amesema lengo ni kukuza mchezo huo na utalii nchini, huku akiamini litakuwa na matokeo mazuri katika sekta hiyo kwa sababu lina manufaa makubwa.

“Tangu Tanzania tumepata Uhuru hii ni mara ya kwanza kufanya shindano hili. Hatutaishia hapa bali litakuwa ni endelevu na litafanyika kila mwaka mwezi Aprili.

Katibu wa mashindano wa Chama cha Gofu Tanzania , Enock Magile akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Hili shindano pia linajumuisha ile kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ya Royal Tour kwa hiyo Golf imekuwa ni ‘product’ kubwa na nzuri kwenye mambo ya utalii, ” amesema Martin.

Amefafanua kuwa wanafanyia kwenye uwanja wa Kilimanjaro Golf Estate kwa sababu ndiyo umekizi viwango vya Kimataifa na maandalizi yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na Serikali.

Kwa upande wake Katibu wa Mashindano wa TGU, Enock Magile, ameeleza kuwa vigezo vya washiriki ni wale wenye viwango vya juu, huku akisema Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kila moja inatoa wachezaji wawili.

Akizungumza kwa niaba ya wadhamini wa mashindano hayo, Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Lumuli Minga, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushudia michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles