24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

DC Maswa aiomba Serikali kuajiri Maafisa Ugani sekta ya mifugo

Na Samwel Mwanga, Maswa

SERIKALI imeombwa kuona uwezekano wa kutoa kibali cha kuajili maafisa Ugani wa Mifugo ili kuweza kuboresha sekta hiyo muhimu katika kuipatia nchi kipato kwa kuuza mazao ya mifugo nje ya nchi.

Hayo yameelezwa leo Jaumatano Machi 23, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge wakati wa ugawaji wa pikipiki tatu zilizotolewa na serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Aswege Kaminyoge akiendesha moja ya pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa Maafisa Ugani sekta ya mifugo wilayani humo huku baadhi ya Wakuu wa Idara za halmashauri ya wilaya hiyo wakishuhudia.

Kaminyoge amesema pamoja na kazi kubwa inayofanyika ya kuboresha sekta hiyo ya mifugo, bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya maafisa ugani na kutolea mfano kwa wilaya ya Maswa ambayo ina Kata 36, Vijiji 120 na vitongoji 510 lakini ina Maafisa Ugani 20 tu.

Amesema wilaya hiyo kwa sasa ina upungufu mkubwa wa Maafisa hao ambao wanashindwa kuwahudumia wafugaji wote waliomo ndani ya wilaya ya Maswa kutokana na upungufu huo.

Amesema moja ya athari ya upungufu huo imesababisha wafugaji wengi ambao wamekuwa wakifuga kiholela kutokana na kutofikiwa na Maafisa Ugani hivyo kushindwa kufuga kibiashara kutokana na kukosa elimu hiyo.

“Uhitaji wa maafisa ugani, uhitaji ni mkubwa, tunaomba serikali iwaajiri maafisa hawa ili waje kusaidia wafugaji wetu huku tulipo maana wengi wao hawapati elimu kwani tunahitaji wafuge kibiashara,”amesema Kaminyonge.

Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo kuipongeza wizara ya mifugo na uvuvi kwa kuanzisha mnada wa Upili katika mji wa Malampaka uliko katika wilaya hiyo na kuwaomba kuanzisha machinjio ya kisasa kwani eneo hilo kuna ujenzi wa kituo cha reli ya kisasa(SGR).

Awali Afisa Mifugo na Uvuvi katika halmashauri ya wilaya hiyo, Dk. James Kawamala akitoa taarifa ya idara hiyo kwa mkuu huyo wa wilaya amesema serikali ilinunua pikipiki 300 kwa ajili ya maafisa ugani wa sekta ya mifugo nchi nzima na katika mgao huo halmashauri ya wilaya hiyo ilipatiwa pikipiki tatu.

Amesema kuwa maafisa ugani hao waliopo kwenye wilaya hiyo ni wachache hasa ukilinganisha uwiano unaotakiwa wa mtaalam mmoja kwa kaya 300 za wafugaji hivyo wilaya hiyo inahitaji Mmaafisa ugani 208 kulinganisha na waliopo ambao ni 20 na hivyo kufanya kuwa na upungufu wa maafisa ugani 188.

Dk. Kawamala amesema kuongezeka kwa pikipiki hizo kutawasaidia maafisa ugani kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo yao na kuwapatia huduma na elimu mbalimbali katika sekta hiyo licha ya kuwepo kwa pikipiki 13 kwa sasa zinazotumiwa na zilizo nyingi no mbovu.

Aidha amewataka maafisa ugani hao waliopatiea pikipiki hizo kuhakikisha wanazitumia vyema ili kuwasaidia wafugaji kufanya ufugaji wenye tija.

Naye Afisa Ugani, Salum Mazige ambaye ni miongoni mwa waliopatiwa pikipiki hizo amehaidi kuitumia kama malengo yaliyokusudiwa ya kuwarahisishia kazi ya kuwahudumia wafugaji katika eneo la wilaya hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles