22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wanusa ufisadi

Rajab-Mohamed-MbaroukElizabeth Hombo na Shabaan Matutu
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imebaini ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 1.7 katika Jiji la Dar es Salaam.
Kutokana na hilo, kamati hiyo imeitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kufuatilia suala hilo pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wote waliohusika.
Pia kamati hiyo imeikataa taarifa ya mkurugenzi wa jiji hilo, Wilson Kabwe kuhusu makusanyo ya fedha za maegesho ya magari kwa kuwa haiendani na uhalisia wa idadi ya magari yaliyopo katika jiji hilo.
Hayo yalibainishwa jana jijini hapa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kukagua miradi iliyofanywa na Kamati ya LAAC na watendaji wa jiji hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mohamed Mbarouk alisema fedha hizo zimetumika kuendesha mradi hewa wa kujenga machinjio ya kisasa ambao una dalili za kifisadi.
“Haiwezekani mradi uanzishwe kwa ubia kati ya Halmashauri tatu na kila mmoja atoe fedha halafu zitumike zote bila hata kuzalisha kipande kimoja cha nyama…lakini mradi ungekamilika ungewasaidia vijana wetu kupata ajira.
“Hii inaweza ikawa Escrow nyingine na kuna tatizo kubwa hapa, sasa tunaiomba TAMISEMI iliangalie suala hili na hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wote waliohusika na ufisadi huu,”alisema Mborouk.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo, Dk. Omary Nundu, alisema anashangazwa na hatua ya meneja, watumishi kupatikana na fedha zote kulipwa wakati bado mradi wa DART haujaanza.
“Hii kweli ni hatari katika hili tunaomba taarifa zaidi, tunataka kujua mchakato ulifanyikaje na nani aliyehusika lakini kwa kusema Sh bilioni 1.7 mlichanga na zote zimetumika halafu tunaambiwa eti hoja hii ifungwe itakuwa ngumu,”alisema Nundu.
Akizungumzia mradi huo, Meya wa Manispaa ya Jiji hilo, Dk. Didas Masaburi alisema suala hilo linalozungumzwa lilipata kutokea miaka kumi iliyopita ambapo aliiomba kamati hiyo kuelewa ufafanuzi wao.
“Sasa kwa kuwa mmetuomba tukae basi tutazingatia maelekezo yenu,”alisema Dk. Masaburi.
Kuhusu taarifa ya maegesho, Mbarouk alisema, “kwa hali ilivyo na uhalisia haiwezekani jiji hilo kupitia halmashauri tatu zikakusanya Sh bilioni 75 pekee, wakati gari zinazoingia na kutoka ni nyingi, kaeni pamoja muone ni utaratibu gani utatumika,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles