PARIS, UFARANSA
MAELFU ya watu wameandamana katika miji mbalimbali ya mataifa ya Ulaya kupinga unyanyasaji wa kijinsia.
Waandamanaji wapatao 30,000 walijitokeza mjini Paris, Ufaransa na mamia katika mji mkuu wa Hispania, Madrid.
Kwingineko maelfu ya watu pia walijitokeza katikati ya mvua mjini Roma, Italia huku maandamano kama hayo pia yakifanyika katika miji ya Geneva, Uswisi na Athens, Ugiriki.
Yote hayo ni sehemu ya kuelekea Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake ambayo ni jana.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameyaunga mkono maandamano hayo na kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa vita dhidi ya unyanyasaji wa wanawake vinaendelea kila siku lakini jamii zetu bado zina kazi kubwa ya kufanya, na kila mtu lazima achukue hatua kwani ni wajibu wa kila mtu.”