24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Vyama 1,268 vyafutwa

msemajiJohanes Respichius na Elizabeth Nyambele, Dar es Salaam

SERIKALI imevifuta vyama vya kijamii 1,268 katika daftari la msajili wa vyama kwa kushindwa kutimiza masharti ya usajili wake.

Taarifa ya kufutwa kwa vyama hivyo ilitolewa jana na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Issac Nantanga, mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

Alisema kazi ya kuhakiki vyama hivyo ina lengo la kufuta vyama vyote vilivyoshindwa kutekeleza masharti ya sheria ya vyama (Sura ya 337) ya mwaka 2002 kuhusu kulipa ada za mwaka.

Nantanga alisema vyama vya kijamii kwa mujibu wa sheria vinapaswa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu za chama vyao na taarifa ya mapato na matumizi kwa msajili.

“Uhakiki huu umehusisha vyama 12,665 ambavyo vimesajiliwa katika daftari la msajili wa vyama na Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi ambapo tangu uanze vyama 1,268 vimefutwa na vingine 312 vimeridhia masharti ya sheria ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’s),” alisema Nyantanga.

Alivita miongoni mwa vyama hivyo kuwa ni pamoja na Lake Victoria Fish Processors Association, Baraza Kuu la Wazee Tanzania, Chama cha Wasafiri Tanzania, NBC Club, Chama cha Wakala wa Mabasi (CHAWAMAKI), Tanzania Techinicans Association (TATEA) na vingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles