22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wazidi kuhama CCM

Chama-Cha-MapinduziSafina Sarwatt (Kilimanjaro) na Eliya Mbonea (Monduli)

IDADI ya viongozi wanaohama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imezidi kuongezeka na jana Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho, Fredrick Mushi, walitangaza kuchukua uamuzi huo, wakifuata nyayo za Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Jana hiyo hiyo mabalozi 110 wa nyumba 10, makatibu wa tawi wanne, wajumbe 11 wa Kamati ya Siasa na Wenyeviti wanne wa Serikali za Mitaa wa CCM, Kata ya Monduli Mjini, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha nao walitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema.

Tangu mchakato wa kumpata mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umalizike mjini Dodoma Julai, mwaka huu na kuacha manung’uniko mengi kutokana na hatua ya vikao vya juu vya chama hicho kulikata jina la Lowassa kimizengwe, kumekuwa na wimbi kubwa la viongozi wanaohama chama hicho.

Hadi kufikia jana viongozi zaidi ya 150 wa ngazi tofauti za uwaziri, ubunge, udiwani na wenyeviti na mabalozi wamekihama chama hicho na kujiunga na Chadema.

Miongoni mwa waliojiunga na Chadema ni pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Arumeru-Magharibi-CCM, Ole-Medeye, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, aliyekuwa Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba, Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya na Mbunge wa Kahama, James Lembeli.

Wengine ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, madiwani 18 wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kupitia CCM, madiwani 20 na Wenyeviti wa vijiji sita wa chama hicho kutoka Jimbo la Monduli.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Nyumbani Hotel, Matemu, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa mkoani hapa, alisema amechoshwa na siasa za CCM, kwani zimejaa mizwenge na fitina na kuwa kama chama cha familia.

Alisema sababu nyingine ya kuondoka kwake CCM ni kile alichokiita kutokutendewa haki kwa mgombea urais ambaye hakumtaja jina kwa kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho pasipo kupewa hata nafasi ya kupigiwa kura, kitendo alichokiita cha uonevu.

“CCM kwa sasa kimegeuka kuwa chama cha familia na wanachama tumekuwa tukiyumbishwa, kwa mantiki hiyo, mimi kwa upeo wangu nimeamua kuhama na kuhamia Chadema ili kupambana na CCM kukiondoa madarakani,” alisema Matemu.

Katika hatua nyingine, Matemu alisema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa jana na Jeshi la Polisi cha kuzuia msafara wa Lowassa, aliyekwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mwasisi wa TANU na CCM, Peter Kisumo.

“Tunalaani kitendo cha msafara wa Lowassa kuzuiwa, kwani ni udhalilishaji kwa mtu aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi, jambo hili linaonyesha dhahiri kwamba kuna mipango ilisukwa kuzuia msafara huo kwa kuhofia nguvu aliyonayo Lowassa kwa wananchi,” alisema Matemu.

Naye Mushi katika mkutano huo alisema ameondoka CCM kutokana na kuchoshwa na

uonevu unaofanywa dhidi ya wanachama wanyonge, huku akidai kuwa haijawahi kutokea Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanagombea wasifanikiwe kuingia hatua ya tano bora.

Mushi alisema hali hiyo inaonyesha CCM iliyopo sasa siyo ile ya zamani, kutokana na kupoteza dira na mwelekeo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles