27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi jeshi, Rais Biden watupiana mpira

VIONGOZI waandamizi wa jeshi la Marekani wamelielezea Bunge kuwa walimshahuri Rais wa nchi hiyo, Joe Biden, kubakiza wanajeshi 2,500 nchini Afghanistan, wazo ambalo hata hivyo halikufanyiwa kazi.

Hata hivyo, wakati wao wakija na utetezi huo kipindi hiki wanapokosolewa vikali kwa hatua ya kuondoa wanajeshi wote Afghanistan, Rais Biden amedai kutokumbuka kama aliwahi kupewa ushahuri wa aina hiyo.

Jenerali Mark Milley na Jenerali Frank McKenzie wamesema walipendekeza Marekani ibakize wanajeshi 2500 na si kuondosha wote kama ilivyotokea na kulilipa nguvu Kundi la Taliban lililoingia madarakani na sasa linaitawala upya Afghanistan.

Itakumbukwa kuwa waandamizi hao wamekuwa kwenye wakati mgumu, wakikosolewa kwa hatua ya Marekani kuondosha wanajeshi waliokuwa wanakabiliana na Taliban.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles