28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Chanjo kupukutisha ajira Marekani

TAKRIBANI waajiriwa 600 wa mashirika ya ndege nchini Marekani watapoteza ajira endapo watashindwa kuendana na sera ya kukabiliana na Corona inayomtaka kila mmoja wao kupata chanjo.

Katika kunusuru ajira zao, tayari wafanyakazi 67,000 wameshawasilisha vyeti vya kuthibtisha kuwa wameshachanjwa, agizo walilotakiwa kulifanyia kazi kufikia Jumatatu ya wiki hii.

Huku hali ikiwa hivyo, bado wapo wenzao 593 ambao huenda wakapoteza kazi kwa kuwa walikataa chanjo kwa minajili ya imani za dini zao na sababu zinginezo.

Wakati hao wakionekana kuwa hatarini kupoteza ajira, idadi ya maombi ya kazi za uhudumu wa ndege zimeendelea kumiminika kwenye mashirika hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles