25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Chadema wagoma kujibu lolote mahakamani, Wakili wa Msigwa ajitoa

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam



Wakili Jamhuri Johnson, anayemtetea Mchungaji Peter Msigwa, katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, ametangaza kujiondoa kumtetea kwa madai ya kutorishishwa na mwenendo wa kesi hiyo unavyoendeshwa.

Wakili Johnson ametangaza uamuzi huo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Alhamisi Novemba 8, mara baada ya upande wa mashtaka kumaliza kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Akitangaza kujitoa kumtetea Msigwa, wakili Johnson amedai haridhishwi na mwenendo wa kesi hiyo jinsi unavyoendeshwa.

Amedai kwa miaka 20 ya uwakili wake, hajawahi kuona kesi inaendeshwa kama inavyoendeshwa hiyo.

Awali, washtakiwa hao wamesomewa maelezo ya awali huku washtakiwa hao wakigoma kujibu lolote wakidai wakili wao hayupo.

Mdhamini wa Ester Matiko ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa amepata ziara ya kibunge na yuko nchini Burundi pamoja na kuwasilisha vielelezo ikiwamo tiketi ya ndege.

Mdhamini wa mshtakiwa wa kwanza, Freeman Mbowe, ameieleza mahakama kuwa bado yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles