25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Kigogo IPTL ahojiwa upya

Kulwa Mzee, Dar es SalaamWakili wa Serikali kutok Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, amedai mahakamani kwamba wamemaliza kumhoji kigogo wa IPTL, Harbinder Sethi baada ya kuomba mahakamani kufanya hivyo.

Swai amedai hayo leo Alhamisi Novemba  8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo inatajwa.

Alidai upelelezi wa kesi hiyo ya kutakatisha fedha inayomkabili Sethi na James Rugemarila haujakamilika isipokuwa walipata nafasi ya kumuhoji Sethi.

Swai aliomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kesi kutajwa na upelelezi unaendelea.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 22 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Watuhumiwa hao bado wanaendelea kusota rumande

Mwisho

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,897FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles