23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Amcos Simiyu kushtakiwa

Na Derick Milton, Maswa.

SERIKALI mkoani Simiyu imesema kuwa itawachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani na kuwashtaki viongozi wote wa Vyama Msingi vya Ushirika(Amcos) watakaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za wakulima wa pamba.

Amesema hataishia kuwavua uongozi na kuwataka kurudisha fedha pekee, pia atawafungulia kesi za wizi lengo ni kukomesha tatizo hilo ambalo limezoeleka na limekuwa likifanywa na viongozi wengi wa Amcos mara nyingi bila hofu yeyote.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ametoa onyo hilo wakati akizungumza na watendaji wa vijiji, kata na tarafa wa Wilaya ya Maswa katika kikao cha mpango mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba msimu wa mwaka 2021/2022.

Kafulila amesema kuwa mara nyingi viongozi wanaofanya ubadhirifu wamezoea kuona wakiambiwa kurudisha fedha na kuvuliwa madaraka na kesi kuishia hapo jambo linalowafanya kuona wizi ni kitu cha kawaida na kwamba ili kukomesha tatizo hilo lazima sheria zitumike .

“Nafasi ya kuendelea kufanya mlivyozoea kwenye Amcos mnaiba kisha unatokomea kusikojulikana ukikamatwa unarudisha na unaendelea nafasi hiyo imefutika, lazima niwaambie ukweli napenda sana ushirika kwa sababu unaunganisha watu wasio na mitaji kupata mitaji lakini ninachukia sana wizi.

“Amcos ikikutwa imefanya ubadhirifu ni mambo matatu, wanarudisha fedha  ndani ya wiki mbili na baada ya kurudisha washitakiwe na uongozi waupoteze ,utamaduni wa kufikiri kwamba kwenye ushirika unachukua hela ukikamatwa unarudisha na biashara inaishia hapo. Takukuru mtu anayekamatwa amefanya wizi ni mambo yote matatu asiishie kurudisha tu,”Amesisitiza Kafulila.

Katika hatua nyingine amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kwenda kufanya operesheni kwa wakulima ya kuchukua hatua  za kisheria  kwa ambao bado wameshindwa kutoa masalia ya pamba ya msimu uliopita na kusambaza samadi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyonge amemhakikishia mkuu wa mkoa kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa hasa mpango mkakati ili kufanikisha lengo la serikali la kuongeza tija na uzalishaji wa zao la pamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles