27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mkuu wa mkoa abaini ‘upigaji’ ujenzi kituo cha afya

Na Mwandishi Wetu, Rukwa

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti  amesema hajaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa kituo kipya cha afya cha Kasu wilayani Nkasi  baada ya kubaini matumizi yasiyo sahihi ya sh  milioni 60 zilizotumika kati ya milioni 500 za kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

Mkiriti ametoa kauli hiyo leo Oktoba 21,2021 wakati alipoanza ziara ya kazi kukagua miradi ya maendeleo na kuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, William Mwakalambile kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za serikali.

“Sijafurahishwa na mwenendo wa kazi ya ujenzi hapa. Inaonekana hapa halmashauri hamjajipanga kukamilisha mradi huu unaosubiriwa mno na wananchi” amesema Mkirikiti

Ameeleza kuwa serikali imetoa milioni 500 kwa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha Afya Kata ya Kasu ambapo tayari kimeanza kwa halmshauri kukusanya vifaa vya kazi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijuakali, amesema ataendelea kuhakikisha watendaji wa halmashauri  wanazingatia matumizi sahihi ya fedha za umma huku miradi ikiwa bora.

“Nilifika hapa awali na kubaini matumizi ya shilingi milioni 60 kinyume cha utaratibu kwani jengo hilo wanalodai ni OPD lilianzishwa na wananchi tofauti na fedha za serikali milioni 500 za sasa hivyo nikaaagiza lisimame,” amesema Lijuakali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles