24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Kilimo kuanzisha kitengo maalum cha kilimo hai

Na Christina Gauluhanga, Mtanzania Digital

WIZARA ya Kilimo nchini imesema imejipanga kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuanzisha kitengo maalum cha kushughulikia kilimo hai na kutenga bajeti maalum ya kilimo hai katika mwaka ujao wa fedha kwa upande wa Bara na Visiwani.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Oktoba 21, 2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa pili wa Kilimo Hai uliofanyika jijini hapa na kuhudhuriwa na wadau zaidi ya 300 wa kilimo hai ulioandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Hai (TOAM) na wadau wa maendeleo.

Pia amesema wizara hiyo imelenga kuanzisha benki maalum ya mbegu za asili ili kusaidia upatikanaji na usambazaji wa mbegu hizo kwa urahisi kwa wakulima nchini.

Bashe amesema pia wizara hiyo itahakikisha Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania TARI) inaanza kufanya utafiti wa mbegu za asili,kuzihifadhi na kuzizalisha ili ziweze kupatikana kwa wingi na gharama nafuu.

“Ili kuhakikisha tunafikia malengo yetu katika kilimo sekta hii na kuimarisha kilimo hai ni lazima pia kuanza kutumia Pareto kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao na kuachana na viwatilifu ambavyo vina kemilikali,” amesema Bashe.

Amesema serikali itahakikisha kilimo hai ufugaji,ardhi ,maji na maeneo mengine yanafuatiliwa na kitengenezewa mazingira rafiki kwa afya ya binadamu kwakuwa ni muhimu kwa maisha na inasaidia katika kukabiliana na magonjwa kutokana na ulaji salama na kutunza mazingira.

“Wizara imewema mikakati ambayo itasaidia kuendeleza kilimo hai kwani ndicho chenye soko tofautu na ile aina nyingine ya kilimo na ulaji wa mazao haya ni dawa ya magonjwa mbalimbali, “amesema Bashe.

Amesema wizara hiyo itaanzieha kitengo maalum cha kilimo hai ambacho kitafanya kazi kwa kushirikiana na wadau ili kuwa endelevu nyakati zote wizarani.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa kilimo hai kuanzia sasa atakuwa balozi wa kilimo hicho.

Amesisitiza kuwa mwaka ujao wa fedha 2021/2022 wataanza kutenga bejeti maalum ya serikali kwa ajili ya kuendeleza kilimo hicho muhimu na TARI itaanza kufanya utafiti wa maendeleo ya kilimo hicho kuwa kuanza na kutafiti mbegu za asili kuzihifadhi na kuzisafisha ili ziweze kupatikana kwa urahisi na gharama nafuu.

Ameahidi kuhakikisha mbegu za asili ambazo kwa sasa hazipatikani kwa urahisi,wataanzisha benki ya mbegu za asili nchini na kuwa na mfumo wa kurejesha mbegu hizo shambani kwa kuzisafisha na kuhifadhi.

“Kusafisha na kuhifadhi mbegu itasaidia kua na mbegu zenye matokeo mazuri na kupata mazao ambayo yatasaidia watanzania kuuza na kupata faida ,kulinda asili ya nchi pamoja na afya za watanzania na dunia, ” amesema Bashe.

Amesema ili.kutekeleza mikakati hiyo kwa kuanzia amemuagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto na TARI kuanza kuangalia namna ya kutafiti na kuanza kutumia zao la pareto nchini ili liweze kutumika kuhifadhia mazao yasishambuliwe na wadudu na kupunguza gharama zaa kutumia viwatilifu vyenye kemikali pamoja na kulinda afya za walaji.

Kwa upande wake ,Waziri wa Kilimo Zanzibar , Soud Nahodha Hassan amesema mpaka sasa mazao yanayozalisha katika visiwa hivyo asilimia 60 ni ya kilimo hai lakini miaka yote wamekuwa wakifadhiliwa na wadau kutoka nje ya nchi na kwa sasa Serikali imedhamiria kutenga bajeti ya kilimo hicho kwa mwaka ujao wa fedha.

Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa na TOAM kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo ubalozi wa Ufaransa,Umoja wa Ulaya EU),Shirika la Umoja wa mataifa la Chakula WFP) na wengineo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles