27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Victor Joseph bingwa Arusha Open 2021

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mashindano ya gofu ya wazi ‘Arusha open 2021’ yamemalizika leo Oktoba 18, 2021 ambapo mchezaji Victor Joseph akiibuka kinara, huku klabu ya Lugalo ikitamba katika  divisheni A.

Victora ambaye ni mchezaji wa klabu ya Dar es Salaam Gymkhana ameibuka mshindi baada ya kupata mikwaju 77 kwa siku ya kwanza na 81 kwa siku ya pili.

Akizungumza baada ya kupata zawadi amesema licha ya ushindi huo amekumbana na changamoto ya mitego uwanjani hali iliyomfanya kupata matokeo ambayo hayakumridhisha pamoja na kutwaa ubingwa.

Kwa upande wa diviaheni A, wachezaji Nicholaus Chitanda wa Lugalo  ameibuka mshindi  baada ya kupata mikwaju ya jumla 153 akifuatiwa na Samwel Kileo naye wa Lugalo  aliyepata mikwaju   ya jumla 159.

Mashindano hayo ya siku mbili yalikutanisha wachezaji zaidi ya 100 kutoka klabu za Dar es Salaam Gymkhana,  Lugalo,  TPC,  Moshi,  Kili, Arusha Gymkhana na klabu za nchini Kenya Machakosi na Muthaiga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles