22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Rufiji amshukuru Rais Samia fedha za maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Rufuji

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, John Kayombo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia halmashauri hiyo Sh bilioni 1.350.

Fedha hizo ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mipya ya mpango wa maendeleo ya ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Uviko-19).

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo na miradi iliyoainishwa, Kayombo amesema Sh milioni 720 zitatumika katika ujenzi wa madarasa 36 ya shule za sekondari na Sh milioni 240 kwa ujenzi wa madarasa 12 ya shule shikizi katika halmashauri hiyo.

“Pamoja na hayo pia fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa jengo la dharura ambazo ni Sh milioni 300 na Sh milioni 90 tutazitumia kwenye ujenzi wa nyumba katika cha kutolea huduma za afya katika halmashauri yetu.

“Kwa mchanganuo huo tunapata jumla ya fedha zote tulizopewa na Rais Samia kuwa Sh bilioni 1.350, tunamshukuru sana na tunatarajia kuzitumia fedha hizo katika miradi iliyokusudiwa,” amesema Kayombo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles